IQNA

Watetezi wa Palestina

Mkuu wa  chama cha Kiislamu cha Tunisia apongeza Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, asema ni zawadi kwa Umma wa Kiislamu

13:37 - November 23, 2023
Habari ID: 3477934
TUNIS (IQNA) - Rached Ghannouchi, mkuu wa Chama cha Ennahda cha Tunisia, alielezea Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kama zawadi kwa Umma wa Kiislamu.

Alielezea Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilitekelezwa na harakati ya Kiislamu ya kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas, dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba iki ni jibu halali kwa ukatili ambao utawala haramu wa Israel umekuwa ukifanya dhidi ya Wapalestina kwa miongo saba pamoja na vitendo vyake vya kuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem).

Katika ujumbe kutoka gerezani, ambao ulichapishwa na bintiye, Ghannouchi alisema operesheni hiyo ni nguvu ya uamsho, motisha, mwamko, na ufahamu na kauli mbiu ya ushujaa wa Umma wa Kiislamu.

Alisisitiza kwamba Msikiti wa Al-Aqsa na Msikiti Mkuu huko Makka na Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina ni maeneo muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu na nyoyo za Ummah na vitisho vyovyote dhidi ya maeneo hayo lazima vikabiliwe na wote.

Ghannouchi alizitaja juhudi za ukombozi wa Palestina kuwa njia ya kupata nguvu Umma wa Kiislamu.

Viongozi wote wa ulimwengu wa Kiislamu watapata mwinuko kwa kuinua bendera ya ukombozi wa Palestina, alisema.

Alisisitiza kwamba suala la Palestina lazima libaki kuwa suala nambari moja la ulimwengu wa Kiislamu.

Ghannouchi, 82, alikamatwa Aprili 17, wakati polisi wa Tunisia walipovamia na kupekua nyumba yake katika mji mkuu wa Tunis kabla ya kumchukua. Kukamatwa huko kulikuja baada ya kuonya kwamba kuondoa mitazamo tofauti kama vile Uislamu wa kushoto au wa kisiasa kunaweza kusababisha "vita vya wenyewe kwa wenyewe" katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.

Tangu mapema Februari, mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imewakamata zaidi ya wapinzani 20 wa Rais aliye madarakani Kais Saied, wakiwemo wanasiasa, mawaziri wa zamani, wafanyabiashara, wana vyama vya wafanyakazi, na mmiliki wa kituo maarufu cha redio cha Tunisia, Mosaique FM.

Mnamo Mei, Ghannouchi, ambaye alikuwa spika wa bunge la Tunisia kabla ya Saied kulivunja Machi mwaka jana, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi, ambayo anayakanusha vikali.

Ghannouchi, mwanzilishi mwenza wa chama cha Ennahda na mkosoaji mashuhuri wa Saied, alianza mgomo wake wa siku tatu wa kula siku ya Ijumaa, na kuahidi kwamba hatakula hadi vikwazo dhidi yake na wafungwa wengine viondolewe.

4183649

Habari zinazohusiana
captcha